Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s).

Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili.

Majlisi hiyo imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Dahani, Dokta Nawaal Aaidi Almayali, wahadhiri wa chuo na wanafunzi, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Shekhe Wasaam Sibti, ikafuatiwa na muhadhara wa kidini kutoka kwa Sayyid Jafari Muruji.

Muhadhara umeeleza utukufu wa bibi Zaharaa (a.s) na nafasi yake mbele ya Mtume (s.a.w.w), akafafanua safari ya Maisha yake (a.s) kwa mujibu wa hadithi za Mtume (s.a.w.w).

Akaeleza pia dhulma aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) baada ya kifo cha baba yake, na namna alivyo simama imara kupigania bendera ya Utume na Uimamu, hakika alimpigania baba yake na mume wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: