Majmaa-Ilmi inajiandaa kutoa nakala ya hati ya Alkafeel

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inajiandaa kutoa nakala ya hati ya Alkafeel.

Itatangazwa rasmi siku ya Jumatatu ijayo (4/12/2023) saa nane mchana kwenye ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hati ya Alkafeel imeandaliwa kwenye kompyuta kupitia program maalum ya uchapishaji wa msahafu chini ya Majmaa, imekidhi vigezo vya hati za kiarabu.

Mpangiliaji wa wati Muhandisi Hussein Ali Shamikhi amesema “Ukamilishaji wa hati umechukua miezi kadhaa, kazi ya kuitengeneza hati katika ubora huu ili iweze kutumika kwenye Qur’ani tukufu”.

Akaendelea kusema “Hati ni miongoni mwa fani za Qur’ani tukufu na jambo kubwa kwa Atabatu Abbasiyya, tumeitengenezea program kupitia mfumo maalum”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: