Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wasichana limeandaa safari ya kidini kwa wanafunzi wake.

Maahadi ya Qur’ani tawi la wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa safari ya kidini kwa wanafunzi wake (100).

Mkuu wa tawi hilo bibi Sinaa Kaadhim amesema “Safari itahusisha wanafunzi (100), watapata chakula katika shamba la mfano la mikunazi na watakwenda kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Safari hii ni sehemu ya kushajihisha wanafunzi waendelee kusoma na kuhifadhi Qur’ani tukufu”.

Maahadi huandaa safari za kidini, semina za Qur’ani, warsha na mihadhara kwa wanafunzi, ili kuwajengea uwezo na kuendeleza vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: