Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Qassim (a.s) mbele ya malalo yake katika mji wa Baabil.

Maukibu ya watu wa Karbala, imeomboleza kifo cha Qassim mtoto wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) mbele ya malalo yake tukufu katika mkoa wa Baabil.

Rais wa kitengo cha Maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil amesema, Mawakibu za watu wa Karbala zimekusanyika kwa kushirikiana na kitengo cha Maadhimisho na Mawakibu Husseiniyya na kuunda Maukibu moja kubwa inayowakilisha watu wa Karbala, wametoa pole kwa msiba huu mkubwa katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wa kifo cha Qassim mtoto wa Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s).

Akaongeza kuwa “Maukibu ya watu wa Karbala imefanya Majlisi ya kuomboleza iliyo hudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru na waombolezaji ndani ya malalo tukufu”.

Makamo katibu mkuu wa mazaru ya Qassim (a.s) Shekhe Ahmadi Jubairi amesema “Maukibu ya watu wa Karbala huja kuomboleza msiba huu kila mwaka” akabainisha kuwa “Wakazi wa mji wa Qassim (s.a) husubiri Maukibu ya watu wa Karbala kwa hamu, kwani tenzi na qaswida huimbwa kwa mahadhi ya Karbala yenye kuhuzunisha”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: