Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) katika nchi ya Mauritania.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya, Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema kuwa, “Majlisi imefanywa kwa ajili ya kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s) na kuangazia utukufu wa Bibi Zaharaa (a.s) na dhulma aliyofanyiwa, akasema kuwa muwakilishi wa Markazi Shekhe Muhammad Faal ameeleza historia ya Bibi Fatuma Zaharaa na utukufu wake, sambamba na kutoa mifano ya elimu, ufasaha na hekima yake (a.s)”.
Shekhe Muhammad Faal amesema kuwa, “Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Mauritania wamefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s) kwa ufadhili wa Markazi Dirasaati Afriqiyya iliyopo chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, akasema dhulma aliyofanyiwa Bibi Zaharaa hasa kumnyima mirathi na shamba la Fadak ni kuwavunjia heshima Ahlulbait (a.s)”.
Mwisho wa Majlisi, wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wakasoma ziara ya bibi Fatuma na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).