Atabatu Abbasiyya inapokea mawakibu za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Atabatu Abbasiyya inapokea mawakibu za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Maukibu za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) zimekuja kumpa pole bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala.

Mawakibu zimefanya matembezi huku zikiimba qaswida za kuomboleza, zimeingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha zikatoka na kupita katikati ya uwanja wa haram mbili hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s) ambako zimefanya Majlisi ya kuomboleza.

Mawakibu zinaingia kwa kufuata ratiba iliyoandaliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu husseiniyya ili kuepusha msongamano baina yao.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kupokea mawakibu za waombolezaji, sambamba na kuandaa mimbari za kutolea mihadhara na kuendesha Majlisi za kuomboleza katika maeneo tofauti na kubainisha utukufu wa Ummul-Banina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: