Ugeni huo umepokelewa na rais wa uhusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ali Azharu ambaye ameelezea baadhi ya miradi ya kilimo inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Kiongozi wa idara ya viatilifu kutoka wizarani Tokta Ahmadi Shaakir amesema “Miradi ya Atabatu Abbasiyya inasaidia serikali kutoa huduma kwa wananchi”.
Akaongeza kuwa “Kuna maendeleo makubwa ya matumizi ya teknolojia katika sekta ya kilimo na kuwa mfano mwema katika sekta hii, hususan upande wa matumizi ya maji”.
Wageni hao wamepata nafasi ya kuzuru malalo takatifu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).