Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imefanya mahafali ya wahitimu (250) wa semina za usomaji sahihi.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya mahafali ya wahitimu wa semina za usomaji sahihi na hukumu za tajwidi wapatao (250).

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manaar Aljaburi amesema “Baada ya kazi kubwa ya kukusanya mabinti na kuwafundisha masomo ya Qur’ani tukufu kwa njia rahisi, leo tunafanya mahafali ya wahitimu (250) wenye umri tofauti waliokamilisha selebasi ya masomo”.

Akaongeza kuwa “Lengo la mahafali hii ni kushajihisha watu wajitokeze kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na kutengeneza jamii inayoshikamana na Qur’ani tukufu”.

Maahadi huandaa safari za kidini, semina za Qur’ani, warsha na utoaji wa mihadhara endelevu kwa wanafunzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: