Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umeandaa shindano la kitamaduni kuhusu mazazi ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s).
Majina kumi ya washindi yatatangazwa Jumanne ya tarehe (23/1/2024m) saa moja jioni kwenye jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu.
Sharti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa awepo kwenye hafla ya kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), itakayofanywa katika eneo la mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumatano (24/1/2024m) sawa na mwezi (12 Rajabu 1445h), kama mshindi atakuwa na udhuru wa kutohudhuria, anatakiwa afike kwenye ofosi za mali (wahasibu) ndani ya siku (4) toka kutangazwa kwa matokeo hayo, akiwa na kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria.
