Kitengo cha Habari na utamaduni katika AAtabatu Abbasiyya kimefungua kisima kipya nchini Averkosti kupitia mradi wa Saaqi Atwasha Karbala.
Mkuu wa Markazi Dirasaati Afriqiyya Shekhe Saadi Sataari shimri amesema kuwa, “Kisima hiki ni sehemu ya mradi wa kuchimba visima kwenye nchi tofauti za Afrika, kimepewa namba (25), kipo katika mji wa Banduko nchini Averkosti, ni kisima cha kwanza kuchimbwa na Markazi mwaka huu na kimepewa jina la Fatuma binti Asadi (a.s) mama wa kiongozi wa waumini (a.s)”.
Akasema kuwa, “Mradi unatekelezwa na Atabatu Abbasiyya kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na Markazi inafanya kila iwezalo kuendeleza mradi huu katika nchi kumi na tatu za Afrika”.
Akasema kuwa, Atabatu Abbasiyya inatekeleza mradi wa Saaqi Atwasha Karbala ambao ni mradi wa kibinaadamu katika jamii ya waafrika.