Kituo cha utamaduni wa familia kimetoa wito kwa waandishi wa kike washiriki kwenye mashindano ya kuzaliwa kwa Ahlulbait (a.s).

Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya, kimetoa wito kwa waandishi wa kike washiriki kwenye shindano la fani za lugha, linalofanyika kufuatia maadhimisho ya kuzaliwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika mwezi wa Shabani.

Kituo kimetoa wito wa kuandika mambo yanayohusiana na kuzaliwa kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Waandishi wataalikwa kuja kuonyesha walicho Andika kwenye hafla ya kuadhimisha mazazi ya Imamu Mahadi (a.f) tarehe (16 Shabani 1445h sawa na tarehe 27/02/2024m) saa nne asubuhi ndani ya ukumbi wa kituo Barabara ya hospitali ya Hussein (a.s) jengo la kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s).

Kwa wanaopenda kushiriki watume nyaraka zao kupitia link ifuatayo:

https://forms.gle/AVubUiGJYedRxC9f7
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: