Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa pole kwa familia ya Shekhe Muhsin Ali Najafi katika dua ya Arubaini yake nchini Pakistan.
Muwakilishi wa Ataba tukufu Shekhe Nasoro Abbasi Najafi ametoa pole kwa mtoto wa marehemu kwenye kikao cha kuomboleza kifo chake kilichofanywa katika chuo kikuu cha Alkauthar nchini Pakistan.
Majlisi imehudhuriwa na viongozi wa hauza, wakufunzi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za kidini, wawakilishi wa Maraajii-Dini na ugeni kutoka Ataba tukufu, wametoa pole kwa familia ya marehemu, wanafunzi wa chuo kikuu cha Alkauthar na walimu wao.