Idara ya haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeweka maua kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya Imamu Mahadi (a.f).
Kiongozi wa Idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Watumishi wa idara wamekamilisha kazi ya kuweka shada za maua kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Mahadi (a.f)”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa vipengele vya kuhuisha ziara ya Shaabaniyya tukufu, ni kupamba dari la dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka shada za maua pamoja na kubadilisha mazulia ya ndani ya haram tukufu”.
Atabatu Abbasiyya huweka shada za maua mazuri yenye rangi na harufu nzuri juu ya dirisha la kaburi la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia maadhimisho ya matukio matukufu, kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara.