Watumishi wa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea kusahihisha majibu ya washiriki wa shindano la (Njia ya wanaosubiri) la kuhifadhi Dua ya Nudba kwa wasichana.
Kiongozi wa idara bibi Taghrida Tamimi amesema kuwa “Wajumbe wa kike katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea kusahihisha karatasi za mtihani wa shindano la (Njia ya wanaosubiri) la kuhifadhi Dua ya Nubda, awamu ya kwanza, shindano hilo limeratibiwa na idara hiyo katika kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s) kufuantia maadhimisho ya kukumbuka mazazi ya Imamu Mahadi (a.f)”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya kusahihisha hufanywa na kamati ya usahihishaji na uhakiki kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi kutokana na umuhimu wa shindano hilo na athari yake katika jamii”.
Shindano limekua na washiriki zaidi ya (700) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kwa mujibu wa maelezo ya Tamimi.