Sayyid Swafi amepiga picha za ukumbusho na mabinti wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria.

Ratiba ya hafla ya wanafunzi wa shule za Al-Ameed wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sharia, imepambwa na upigaji wa picha za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi akiwa na mabinti hao.

Hafla imeratibiwa na kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo (Hijabu ni msingi wa stara na usafi wangu), inawashiriki (770) ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi waliofikisha umri wa kuwajibikiwa na sharia.

Zimepigwa picha za pamoja baada ya wanafunzi kukusanyika kwenye jukwaa kuu huku wanaimba wimbo wa kuwajibikiwa na sharia na wakiwa wameshika mishumaa ya nuru ya kuwajibikiwa na sharia.

Hafla inavipengele tofauti, miongoni mwake ni kuangalia picha ya video inayo elezea mradi wa kuwajibikiwa na sharia (Taklifu), kusoma qaswida na mashairi kutoka kwa mshairi Muhammad Yasiri na kugawa zawadi kwa washiriki
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: