Kitengo cha utamaduni kinaendesha ratiba ya Sufratul-Kafeel katika mji wa Kano nchini Naijeria.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeendesha ratiba ya (Sufratul-Kafeel) katika mji wa Kano nchini Naijeria.

Ratiba imehusisha utoaji wa muhadhara maalum kuhusu mwezi wa Ramadhani wenye anuani isemayo (Umuhimu wa tabia njema katika kulinda jamii).

Ratiba ya Sufratul-Kafeel hupambwa na usomaji wa Qur’ani, mawaidha, mihadhara ya Fiqhi, Aqida na Akhlaq mbele ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao.

Ratiba hiyo imesimamiwa na muwakilishi wa Markazi nchini Naijeria Shekhe Bashiru Thani Mahmuud, ambae ametoa muhadhara wa kimaadili kuhusu kunufaika na mwezi wa Ramadhani kwa kurekebisha tabia ya mtu na jamii, sambamba na kufafanua riwaya zilizopokewa kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) zinazohimiza maadili mema katika kulinda jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: