Chuo kikuu cha Alkafeel kinaendesha ratiba ya mwezi wa Ramadhani katika majengo yake.

Chuo kikuu cha Alkafeel kinaendesha ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani katika majengo yake kwa kushirikiana na kikosi cha Habari.

Wasimamizi wa ratiba hiyo ni kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi (saikolojia) katika chuo, mbele ya walimu, wanafunzi na familia zao.

Ratiba imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Hassan Abbasi, kisha ratiba ikatambulishwa halafu likasomwa shairi na mwanafunzi Huda Hussein, zikasomwa tenzi, yakafanywa mashindano tofauti, kukawa na maonyesho ya kitamaduni na kielimu pamoja na maonyesho ya igizo.

Siku ya kwanza imeangaliwa filamu yenye anuani isemayo “Saa moja kabla ya sifuri”, imeonyesha mazingira ya kutolewa kwa fatwa ya jihadi kifaya ya kujilinda, pamoja na kujadili mambo mbalimbali yaliyotokea.

Ratiba hiyo itadumu kwa muda wa siku tano mfululizo, jambo ambalo linatoa nafasi kwa wanafunzi kusikia mambo mengi yanayohusiana na mwezi wa Ramadhani na kukaa katika mazingira mazuri kiroho ndani ya mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: