Katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan (a.s).. kimefanywa kikao cha usomaji wa Qur’ani kwenye mji mkuu wa Baghdad.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan (a.s) kwenye mji mkuu wa Baghdad.

Kikao hicho kimefanywa ndani ya Msikiti na Husseiniyya ya (Haajat Fakhariyyah Birimani) kitongoji cha Raswafa katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Ali Namiir, ikafuatiwa na kisomo cha surat Fat-hah kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, halafu Mu’tamadi Marjaiyya Sayyid Imadi-Dini Mussawi akatoa mawaidha.

Hafla imepambwa na kisomo cha Rasuul Daraji, na baadhi ya beti za mashairi kutoka kwa Ali Dhahabi na ikahitimishwa kwa kusoma Dua Faraj.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: