Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya shindano la kiigizo chema awamu ya pili.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimetangaza shindano la (kiigizo chema) awamu ya pili, linalolenga kufundisha historia ya Mtume (s.a.w.w).

Shindano linasimamiwa na Daaru Rasuulul-A’adham chini ya kitengo.

Shindano linamaswali (50) kuhusu historia ya Mtume (s.a.w.w), linalenga kujenga elimu ya kumtambua Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika jamii ya waislamu na kushajihisha kutenga muda kwa ajili ya kusoma historia yake ili kuweza kuiga mwenendo wake mtukufu.

Ushiriki unaanza tarehe 1/4/2024m na mwisho ni tarehe 1/5/2024m, washindi kumi wa mwanzo watapewa zawadi katika hafla itakayofanyika kuadhimisha tukio litakalo teuliwa baadae.

Kwa maelezo zaidi piga namba ifuatayo: 07602355555.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: