Kitengo cha habari na utamaduni kimeandaa ratiba maalum ya kidini katika nchi ya Naijeria.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba maalum ya kidini katika nchi ya Naijeria.

Ratiba hiyo imetekelezwa kupitia mradi wa Sufratul-Kafeel katika mji wa Kano nchini Naijeria, chini ya Markazi Dirasaati Afriqiyya.

Muwakilishi wa Markazi nchini Naijeria Sayyid Bashiru Thani Mahmud amesema “Ratiba imehusisha utoaji wa mihadhara na vikao vya usomaji wa dua za pamoja katika mji wa Kano nchini Naijeria”.

Akaongeza “Mihadhara imejikita katika kufafanua mambo ya kifiqihi na kimaadili pamoja na kubainisha misimamo ya kisheria”.

Akaendelea kusema “Vikao vya usomaji wa dua vimehusisha baadhi ya dua maalum za mwezi wa Ramadhani, kama vile dua Iftitaah, dua Komail na zinginezo miongoni mwa dua muhimu katika kujenga roho ya mwanaadamu”.

Ratiba imejikita katika kuimarisha umoja na kujenga undugu baina ya jamii za kidini kwa wakazi wa mji huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: