Ofisi ya Muheshimiwa Marjaa-Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani imetangaza kuwa kesho siku ya Jumatano ya tarehe 10 Aprili ni siku ya kwanza ya Idul-Fitri.
Ofisi ya Sayyid Sistani imesema “Imethibiti kuandama kwa mwezi kisheria hapa Iraq na maeneo yote ya miji hii, hivyo Jumatano ya kesho ni siku ya kwanza ya Idul-Fiti mwezi mosi Shawwal mwaka 1445h”.
Akaongeza kuwa “Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awakubalie wote funga na swala zao na atupe amani furaha na baraka katika sikukuu hii tukufu”.