Shekhe Karbalai amekuja Atabatu Abbasiyya tukufu kutoa pongezi za Idul-Fitri akiwa na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Hassan Rashidi Al-Abaaiji na baadhi ya viongozi.
Ugeni huo umepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Wamepeana pongezi za Idul-Fitri na kumuomba Mwenyezi Mungu alitunuku taifa la Iraq na raia wake amani na usalama.
Ugeni kutoka Atabatu Husseiniyya ukafanya ziara katika malalo ya Abulfadil Abbasi (a.s) wakiwa pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na makamo wake.
Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea viongozi wengi wa Karbala na raia wa kawaida waliokuja kutoa pongezi za sikukuu.