Msomaji wa Atabatu Abbasiyya amekuwa mshindi wa nne kwenye mashindano ya kimataifa ya “Aya bainifu” yaliyofanyika nchini Lebanon.

Msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Liith Ubaidi amekuwa mshindi wa nne kwenye mashindano ya Qur’ani tukufu yaliyofanyika nchini Lebanon.

Mashindano hayo yaliandaliwa na chanel ya Siraat mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani kwa ushiriki wa nchi (15) ambao wameshindana katika hatia tatu tofauti.

Mwisho wa mashindano yakatangazwa matokeo, ambapo msomaji wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Liith Ubaidi amekuwa mshindi wa nne.

Mashindano ya Qur’ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani huonyesha umuhimu wa kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa kuzingatia usomaji sahihi na tajwidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: