Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaif amesema “Watumishi wa idara yetu wameanza kati ya kusafisha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kutandika mazuria sambamba na kupuliza marashi kwa kufuata ratiba maalum”.
Akaongeza kuwa “Kazi imehusisha kuondoa mazuria ya zamani, kupiga deki, kutandika mazuria mengine na kupuliza marashi”.
Akaendelea kusema “Kazi hizo hufanywa kwa muda maalum, kwa lengo la kuondoa usumbufu kwa mazuwaru watukufu”.