Idara ya maelekezo ya kidini katika Atabatu Abbasiyya, imeomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Idara imeomboleza kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s) kwa kufanya Majlisi ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhidm (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Akaongeza kuwa “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Mwanamke mwema katika uislamu), uliotolewa na mmoja wa wahadhiri kutoka idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake, ameongea sifa za mwanamke mwema kutokana na hadithi za Mtume (s.a.w.w) na majukumu yake”.
Akaendelea kusema “Idara hutilia umuhimu katika kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) kwa wanawake, ili kuweza kufuata mwenendo wao kwa vitendo”.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na mashairi yanayomuhusu Imamu Jafari Swadiq (a.s) na Duau-Faraji.