Jumuiya ya kielimu na kitamaduni Al-Ameed imeshiriki kwenye nadwa ya awamu ya pili iliyopewa jina la (Kuangazia kitabu cha Shakhsiyyatu-Muhammadiyya cha Maarufu Raswafi).
Nadwa imesimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kupitua Daaru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w).
Nadwa imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Muhammad Zubaidi, ikafuatiwa na Surat Fat-hah kwa ajili ya kurehemu mashahidi na wanachuoni, halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Ibaa), kisha mawaidha kutoka kwa Dokta Liith Waailiy makamo rais wa Daaru, amebainisha umuhimu wa nadwa hizi na malengo yake.
Dokta Haamid Abdul-Muhsin Aljanabi akatoa muhadhara na muendeshaji wa kikao alikuwa ni rais wa Daaru Dokta Aadil Nadhiri Biriy.
Mwisho wa Nadwa washindi wa shindano la (Kiigizo chema) wakapewa zawadi, shindano hilo lilikuwa na maswali (50) kuhusu historia ya Mtume Mtukufu.












