Idara ya Fatuma binti Asadi ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha semina ya (Yanabia-Rahmah) iliyokuwa na washiriki karibu 360 kutoka mkoa wa Karbala.
Kiongozi wa Idara bibi Fatuma Mussawi amesema “Hafla ya kufunga semina imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na wanafunzi wa semina na ilikua na vipengele tofauti, miongoni mwa vipengele hivyo ni (Picha na maoni) kilicho simamiwa na kiongozi wa kituo cha utamaduni wa familia, kikafuata kipengele cha (Fikra yangu na jawabu) iliyokuwa na maswali mbalimbali kutoka kwa idara ya Fatuma binti Asadi”.
Akaongeza kuwa “Hafla imepambwa na kaswida kuhusu Ahlubait (a.s) kutoka kwa wanafunzi tofauti wa semina, pamoja na kaswida kuhusu bibi Zainabu (a.s), ikahitimishwa kwa kugawa vyeti vya ushiriki na zawadi za kutabaruku”.
Idara ya Fatuma binti Asadi imeweka umuhimu mkubwa katika kufanya semina za majira ya kiangazi kwa lengo la kufundisha mabinti mambo muhimu katika Dini na utamaduni, yanayosaidia kujenga kizazi chenye elimu bora na maarifa.