Daktari bingwa wa mifupa Dokta Muhandi Shimri amesema kuwa, uwepo wa vifaa-tiba vya kisasa katika hospitali ya rufaa Alkafeel, umerahisisha upasuaji mgumu uliokuwa hauwezekani siku za nyuma.
Akasema kuwa “Vyumba vya upasuaji vinavifaa-tiba vya kisasa, vinavyo tuwezesha kufanya upasuaji kwa urahisi na mafanikio makubwa” akabainisha kuwa “Miongoni mwa upasuaji mgumu tuliofanya ulikuwa wa kijana mweze umri wa miaka ishirini aliyepata ajali na kuumia kwenye uti wa mgongo”.
Akaongeza kuwa “Upasuaji huo ulikuwa hatari, tulifanikiwa kuresha uti wa mgongo katika hali yake na kuunga mifupa iliyokua imevunjika, baada ya matibabu hayo kijana aliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na afya njema”.
