Maelfu ya mazuwaru wanahuisha usiku wa tano wa mwezi wa Muharam katika mji wa Karbala.

Maelfu ya wazuwaru wamehuisha usiku wa tano wa mwezi wa Muharam mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala zimeshuhudia makundi makubwa ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali, tukiwa tunakaribia siku ya mwezi kumi Muharam, siku ambayo waumini huomboleza kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake.

Waombolezaji wanahuisha kumbukumbu ya tukio la kuumiza na kuenzi misingi ya Imamu Hussein (a.s) na kujitolea kwake katika kutetea haki na uadilifu.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein, watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake katika siku ya Ashura.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: