Idara ya Dini inaomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s)

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s).

Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Idara imeomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s) kwa kufanya majlisi ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa Ziaratu-Ashuraa”.

Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na igizo la (Wanaomlilia Hussein –a.s-) lililofanywa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Ataba tukufu, likafuatiwa na qaswida zilizotaja dhulma aliyofanyiwa Imamu (a.s) na ujumbe unaopatikana katika misingi ya Dini tukufu”.

Akaendelea kusema “Watumishi wa idara wameandaa shindano la Naafidhu-Albaswirah kwa mazuwaru na waombolezaji ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), lililokuwa na maswali kuhusu historia ya Imamu Sajjaad (a.s)”.

Idara ya Dini hufanya majlisi ya kuomboleza katika kila tukio la msiba unaohusu Ahlulbait (a.s), kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: