Mji mtukufu wa Karbala umeshuhudia makundi makubwa ya mazuwaru waliokuja kuhuisha usiku wa pili wa mwezi wa Safar mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mji wa Karbala hupokea mamilioni ya watu katika mwezi wa Safar, ambao huja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhuisha utiifu wao kwa Ahlulbait (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia vitengo vyake, hufanya kila kinachowezekana katika kuhudumia mazuwaru na kukidhi mahitaji yao.