Rais wa kitengo hicho, Sayyid Nasoro Hussein Mut’ibu amesema “Vituo vya usambazaji wa maji vimewezesha shughuli za kilimo na kutoa nafasi kwa watumishi wa ukanda wa kijani kibichi kuanza kulima mbogamboga kwa lengo la kunufaika na sehemu za wazi”.
Akaongeza kuwa “Mazao ya aina tofauti yanalimwa katika eneo la ukanda wa kijani, miongoni mwa mazao hayo ni, bilinganya, nyanya na mbogamboga mbalimbali”.
Akabainisha kuwa “Kitengo kinalima mazao hayo kwa lengo la kuyatumia katika mgahawa (mudhifu) wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na mengine kuingizwa sokoni”.