Idara ya Fatuma binti Asadi (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imeendelea na ratiba yake ya kila wiki (Manaahil-Rawiyya).
Ratiba hiyo inafanywa katika kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s), kwenye mazingira tulivu kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kusoma Qur’ani katika jamii.
Ratiba inahusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, Dua Nudba, Qaswida zinazoelezea kutawalishwa Imamu Mahadi (a.s).
Program imehitimishwa kwa kusoma Dua Faraj ya Imamu wa zama (a.f).