Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea kutoa mihadhara kuhusu madhumuni ya Nahajul-Balagha kwa watumishi wa kitengo cha ushauri nasaha katika chuo kikuu cha Al-Ameed.
Mihadhara imejikita katika kueleza mafundisho ya Nahajul-Balagha, kitabu kilichokusanya khutuba za kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) katika sekta ya elimu, itikadi, akhlaqi na jamii.
Mihadhara hii inasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uwelewa kwa washiriki na kujenga uwezo wao katika kuamiliana na watu wengine sambamba na kufuata mafundisho ya Nahajul-Balagha katika maisha ya kila siku.



