Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha majlisi za kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Majlisi ya mwisho ndani ya Ataba tukufu imehudhuriwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na idadi kubwa ya mazuwaru watukufu.
Mzungumzaji alikuwa Shekhe Jaasim Haatimi, ameongea kuhusu utukufu wa Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na akataja dhulma alizofanyiwa, aidha majlisi imepambwa kwa tenzi na qaswida kutoka kwa Ali Saaidi na Hassan Qatwirani.
Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu, yenye vipengele vingi na imedumu kwa muda wa siku tatu.
Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya majlisi za kuomboleza matukio ya misiba ya Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuhuisha utajo wao, kusambaza elimu zao na utukufu wao.







