Idara ya wahadhiri tawi la wanawake imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu-Twahirah (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Majlisi imepambwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Fatuma Zaharaa –a.s- na yaliyonyumba ya Fadak), mzungumzaji amefafanua sababu za Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kuomba apewe Fadak, namna alivyoifanya kuwa anuani ya kurejeshwa haki za waislamu, vipengele muhimu alivyosisitiza kuhusu haki ya Uimamu na Ukhalifa kwa Imamu Ali (a.s) baada ya Mtume (s.a.w.w).

Muhadhara umejikita katika kuelezea namna Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alivyopambana kutetea madhehebu, Aqida na msimamo wake katika wakati huo mgumu.

Idara hufanya majlisi za kuomboleza misiba ya Ahlulbait (a.s) na kuwafundisha wanawake mwenendo wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: