Rais wa washauri wa kilimo katika mradi huo Sayyid Abbasi Muhammad amesema “Watumishi wa mradi wa kijani kibichi wameanza kulima aina tofauti za mbogamboga na mitende, kwa lengo la kuongeza eneo la kijani kibichi, kupambana na jangwa, kulinda mazingira na kuendeleza mradi”.
Akaongeza kuwa “Tumeongeza mitende kwa kupanda miche 3850, tunatarajia kuongeza idadi ya miche hiyo siku zijazo, aidha tumepanda miche 4000 ya mikaratusi upande wa kushoto mwa mradi kwa ajili ya kuzuwia upepo na vumbi”.
Akasema kuwa “Mbogamboga zilizopandwa ni: karoti, shalgham, viazi-damu, spinach, alkalam, kunde, tango, nyanya, vitunguu na ainda zingine nyingi za mbogamboga”.
Akaendelea kusema “Mradi wa kijani kibichi unatumia umeme wa jua katika kuendesha mitambo yake ya umwagiliaji kupitia vituo viwili, kila kimoja kikiwa na mota 10”, akabainisha kuwa “Faida ya kutumia umeme wa jua katika mradi huu, unatuwezesha kufikisha maji mbali”








