Idara ya wahadhiri wa mimbari Husseiniyya tawi la wanawake imefanya program ya wahadhiri wa muungano huo awamu ya sita.

Idara ya wahadhiri wa mimbari Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la sita.

Kiongozi wa idara Bibi Taghridi Tamimi amesema “Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake imefanya program ya muungano huo awamu ya sita, mimbari Husseiniyya inamchango mkubwa katika kurekebisha mtu na jamii, hakika muungano huo ni muhimu sana katika sekta ya tablighi”.

Akaongeza kuwa “Program inahusisha masomo ya Qur’ani, Fiqhi, Aqida, mbinu za utoaji wa mihadhara, mahadhi ya mihadhara inayohusu Imamu Hussein (a.s), mihadhara ya Akhlaq inayoendana na historia ya Ahlulbait (a.s)”, akabainisha kuwa “Masomo yanafundishwa kila siku ya Alkhamisi”.

Akasema kuwa “Wahadhiri wamealikwa kutoka mkoa wa Najafu, Baabil pamoja na wenyeji mkoa wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: