Asubuhi ya Ijumaa kundi la mazuwaru limeshiriki kusoma Dua Nudba ndani ya Maqamu ya Imamu Mahadi (a.f).
Mazuwaru hujitokeza kwa wingi katika eneo hilo takatifu kusoma dua yenye Baraka za Imamu msubiriwa (a.s).
Watumishi wa kitengo huandaa mazingira mazuri na huweka vitabu vya dua sambamba na kupuliza marashi eneo hilo.
Dua huongozwa na mmoja wa wahadhiri wa mimbari Husseiniyya na huduma zingine tofauti hutolewa kwa washiriki ili kuweka mazingira ya kiroho.











