Marjaa-Dini mkuu Sayyid Ali Sistani siku ya Jumatatu, amempokea muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Iraq.
Nakala ya tamko iliyotolewa na ofisi yake inasema:
Muheshimiwa Sayyid Sistani leo kabla ya Adhuhuri, amempokea Dokta Muhammad Hasaan, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na rais wa ujumbe wake nchini Iraq pamoja na ujumbe aliofuatana nao.
Muheshimiwa ameongea kuhusu jukumu la ujumbe wa kimataifa na nafasi yao katika siku zijazo, naye Sayyid Sistani amekaribisha uwepo wa umoja wa mataifa nchini Iraq, na kuwatakia mafanikio mema katika majukumu yao, akaongea kuhusu changamoto kubwa zinazolikabili taifa la Iraq kwa sasa, na matatizo wanayopata raia katika mambo mbalimbali, akawataka wachukue mazingatio katika mambo yaliyopita na wafanye kila wawezalo katika kuboresha maendeleo ya taifa, kila mwananchi ahisi amani na utulivu katika taifa lake, jambo hilo haliwezi kufikiwa bila kuwa na utawala bora katika taifa, kwa kupewa madaraka watu wenye uwezo wa kuongoza taifa na kuzuwia kuingiliwa na mataifa ya nje, kuwe na utawala unaofuata sheria, siraha zote ziwe chini ya serikali, kupambana na ufisadi katika ngazi zote, lakili inaelekea wairaq wanasafari ndefu kufika hapo, Mwenyezi Mungu awasaidie kwa hilo, kuhusu mambo yanayo endelea katika maeneo yetu, mauaji wa kinyama yanayofanywa nchini Lebanon na Gaza, tunasikitika sana kwa umoja wa mataifa na taasisi zake kushindwa kusimamisha mauaji hayo au kuwalinda wananchi wasiokuwa na hatia kutokana na unyama unaofanywa na mazayuni wa Israel.
Ofisi ya Sayyid Sistani Najafu Ashrafu
1 Jamadal-Uula/ 1446h sawa na 4/11/2024m.
