Hospitali ya Atabatu Abbasiyya tukufu nchini Siria, inahudumia wakimbizi 1500 kutoka Lebanon kila siku, kupitia mpango wa kusaidia wakimbizi.
Kiongozi wa madaktari wa Ataba tukufu nchini Siria Sayyid Ahmadi Hussein amesema “Hakika Hospitali yetu inahudumia karibu wakimbizi wa Lebanon 1500 kila siku”.
Akaongeza kuwa “Kutokana na mahitaji ya uwepo wa madaktari na wauguzi kwa ajili ya kutibu wakimbizi, Atabatu Abbasiyya iliitikia wito huo kwa kujenga eneo la kutolea huduma za afya kwa familia za wakimbizi”.
Wakimbizi wamepongeza Atabatu Abbasiyya kwa kuwapa huduma za matibabu pamoja na huduma zingine zinazosaidia kupunguza matatizo ya familia za wakimbizi.
Atabatu Abbasiyya ilifungua hospitali maalum kwa ajili ya kutibu wakimbizi wa Lebanon nchini Siria, baada ya wito wa Marjaa-Dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani aliyehimiza kusaidiwa watu wa Lebanon kwa kuwapa huduma za kibinaadamu baada ya kushambuliwa na utawala wa kizayuni.


