Mkuu wa mkoa wa Karbala amesema: Mradi wa Firdausi ni muhimu katika utunzaji wa mazingira hapa mkoani.

Mkuu wa mkoa wa Karbala Sayyid Naswifu Jaasim Alkhatwabi amesema kuwa mradi wa Firdausi ni muhimu katika utunzaji wa mazingira hapa mkoani na utahudumia familia za wakazi na mazuwaru.

Ameyasema hayo alipohudhuria hafla ya ufunguzi wa mradi huo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akasema kuwa “Mradi unamchango mkubwa wa kutunza mazingira sambamba na maeneo mazuri ya kupumzika familia za watu wa Karbala na mazuwaru”, akasema “Mkoa ulitoa ushirikiano kwa kiwango kikubwa, kwa kutoa ardhi na mahitaji ya lazima katika utendaji”.

Akafafanua kuwa “Mradi huu ni sehemu ya miradi inayotekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Karbala, utachangia kwa kiwango kikubwa kuimarisha sekta ya utalii hapa mkoani”.

Akapongeza kazi kubwa inayofanywa na mafundi wa Atabatu Abbasiyya, na kusisitiza umuhimu wa mradi huu katika kuboresha mazingira ya mkoa kwa kuongeza eneo la kijani kibichi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: