Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya leo siku ya Ijumaa umeshuhudia kundi kubwa la waumini walioshiriki kusoma Dua Nudba.
Usomaji wa Dua umefanywa katika mazingira tulivu ya kiroho na Baraka za mnasibishwaji wa Dua hiyo kwa ushiriki wa idadi kubwa ya mazuwaru wa eneo hili takatifu.
Watumishi wa Ataba wameweka mazingira mazuri kwa usomaji wa Dua, wameweka vitabu vingi vya Dua, wameandaa sehemu maalum, wamepuliza marashi sehemu hiyo, wamepangilia vizuri na kutoa huduma zote zinazohitajika.









