Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Zainabu (a.s).
Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Hibah Ridhwa, ikafuatiwa na muhadhara wenye anuani isemayo (Umuhimu wa mwanamke katika jamii), kutoka kwa kiongozi wa idara ya habari Bibi Rajaa Ali, ameongea kuhusu umuhimu wa kumsoma Bibi Zainabu (a.s) na kutafakari mwenendo wake, hakika yeye ni mfano bora wa kuigwa katika maisha yetu ya kila siku”.
Akaongeza kuwa “Hafla ilikua na vipengele tofauti, ikiwemo kuwapa zawadi wasichana wenye jina la Zainabu, usomaji wa qaswida na mashairi kutoka kwa Zaharaa Hussein, kulikuwa na shindano lenye maswali 10 kuhusu histotia ya Bibi Zainabu (a.s)”.
Akasema kuwa “Idara imeandaa ratiba ya watoto waliokuja na familia zao, kwa lengo la kuwajengea utamaduni wa kidini kupitia picha na upakaji wa rangi, sambamba na kugawa zawadi za tabaruku kwa watoto”.



