Kundi la waumini linashiriki katika usomaji wa Dua Komail mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa, umeshuhudia kundi kubwa la waumini walioshiriki kusoma Dua Komail.

Usomaji wa dua hiyo tukufu umefanywa katika mazingira tulivu ya kiimani, yaliyojaa baraka za mnasibishwa wa dua hiyo na ushiriki wa idadi kubwa ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu huweka mazingira mazuri ya usomaji wa dua, huweka vitabu vya dua na huandaa sehemu maalum ya kufanyia ibada sambamba na kutoa huduma zote zinazohitajika kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: