Mawakibu za kuomboleza zinahuisha kumbukumbu ya kifo cha Bibi Zaharaa (a.s) katika mji wa Karbala.

Mawakibu za kuomboleza zinahuisha kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.

Mmoja wa watu wa mawakibu kutoka mkoa wa Najafu Sayyid Ali Ghazali amesema “Mawakibu za kuomboleza zimemiminika katika mji wa Karbala kutoka mikoa tofauti, katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Katika vipengele vya kuomboleza imehusishwa kushindikiza jeneza ya kuigiza jeneza la Mbora wa wanawake wa duniani (a.s)”, akasema kuwa “Mawakubu zimetoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huo”.

Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeratibu matembezi ya waombolezaji na kurahisisha ufanyaji wa ziara.

Atabatu Abbasiyya huweka mazingira rafiki ya uombolezaji katika kuhuisha kumbukumbu za kifo cha Ahlulbait (a.s) sambamba na kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa malalo mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: