Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameomboleza kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili kwa kufanya maukibu ya pamoja.
Maukibu imeshuhudia uwepo wa wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ashqar, Sayyid Kaadhim Abadah na mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Fadhili Auzi na baadhi ya viongozi wa Ataba mbili tukufu.
Auzi amesema “Mji wa Karbala umeshuhudia idadi kubwa ya mawakibu Husseiniyya zilizokuja kutoa pole kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya pili”.
Akaongeza kuwa “Maukibu imefanya matembezi kuandia ndani ya mamalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita katikati ya uwanja wa haram mbili tukufu huku wakiimba qaswida za kuomboleza zilizoamsha hisia za huzuni na majonzi, wakatembea hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s)”.
Akaendelea kusema “Baada ya kufika katika uwanja wa haram ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wakafanya majlisi ya kuomboleza iliyopambwa na qaswida na mashairi yaliyotaja dhulma aliyofanyiwa mtoto wa Mtume (a.s)”.




















