Wahudumu wa kipindi cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya wanatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kiongozi wa idara ya usafi Sayyid Kadhim Jawaad amesema “Watumishi wa idara husafisha Sardabu za Ataba na kutandika karibu miswala (mazulia) 350, ambayo husafishwa kwa kutumia mitambo, sambamba na kupanga vitabu vya ziara, dua na turba”.
Akaongeza kuwa “Kazi huhusisha usafishaji wa lifti (ngazi) za umeme ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), pamoja na kusafisha madirisha na vioo, na kuandaa sehemu za kuswali jamaa, sehemu za kuendesha semina za kidini, na sehemu maalum kwa ajili ya wanafunzi wanaojisomea”.
Kitengo kupitia watumishi wake kinatoa huduma bora na usafi wa hali ya juu, ili kumpa Amani na utulivu mwenye kuzuru malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).







