Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Muratadha Aalu Dhuyaau-Dini amesema kuwa, sekta ya malezi na elimu ni kipaombele cha Ataba tukufu.
Ameyasema hayo alipohudhuria mahafali ya mwaka wa nne ya wanafunzi wa shule za Al-Ameed katika mwaka wa masomo (2023 – 2024m), iliyoandaliwa na kitengo cha malezi na elimu katika Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo “Al-Ameed inamfurahia mwanafunzi wake mtukufu”.
Muheshimiwa Sayyid Aalu Dhiyaau-Dini amesema, “Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, inajali sana sekta ya malezi na elimu, kuanzia shule za awali hadi vyuo”. Akaongeza kuwa “Kuna mtazamo mpya na juhudu kubwa ya kukamilisha ujumbe wa malezi utakaohakikiwa na Marjaa-Dini mkuu katika mji wa Najafu, utakaokuwa na sekta tofauti zinazo husu maendeleo ya taifa kwenye mambo yote”.
Akatoa wito “Kwa walezi na walimu wote wachangie kuandaa ujumbe wenye maana ya kibinaadamu na kimaadili, na kujali wanafunzi kwa kuwaandaa na kuwawezesha kujenga taifa la Iraq”.
Hafla imehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya, viongozi wa mkoa wa Karbala, mkuu wa idara ya malezi ya mkoa, walimu, wanafunzi na wazazi wa wanafunzi.









