Badri amesema “Muhadhara ulikua na maudhui isemayo (Uongozi wa taasisi za habari, Atabatu Abbasiyya kama mfano), ameongea kuhusu vituo, idara na vitengo vilivyopo katika Ataba tukufu, vinavyo saidia kufikisha ujumbe wake kila sehemu ya Dunia”.
Akaongeza kuwa “Muhadhara huo ni sehemu ya ushirikiano wake na vyuo vikuu vya Iraq, kwa lengo ya kuonyesha kazi zinazofanywa na sekta ya habari katika Atabatu Abbasiyya, mada imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na walimu waliohudhuria”.
Akasisitiza kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu huwavutia sana wafuasi wa Ahlulbait (a.s), jambo linalosababisha kitengo cha habari kutoa ujumbe sahihi kwa umakini mkubwa”.